Mlezi wa
Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege kubwa
yenye uwezo wa kubeba watu 150, lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya ndege
hiyo.
Rahma,
maarufu kama Malkia wa Nyuki, ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320
inayomilikiwa na Serikali ya Oman na anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi
wa Heshima wa Oman nchini Comoro.
| AKIWA NA WAFANYAKAZI WA AIRPORT UPANDE WA VIP NA BINTIYE, NYUKI MTOTO (KULIA) |
| AKIWA NA NYUKI MTOTO |
Ndege hiyo
ilikuwa imebeba watu 17, kati ya hao 16 ni wafanyakazi ndani ya ndege ambao ni daktari
mmoja, walinzi wanne, waliobaki ni marubani na wahudumu.
Akizungumza
dakika chache kabla ya kuondoka nchini jana, saa 10 alfajiri, Malkia wa Nyuki
alisema alishuka nchini kwa ajili ya mapumziko ya siku moja, pia kuzungumza na
baadhi ya viongozi wa Simba.
“Nimepita
tu, tumepumzika kidogo hapa na baada ya hapo ninakwenda Comoro kwa ajili ya
kuzungumza na kumchukua Rais wa Comoro.
| AKIAGANA NA WADAU.. |
“Lakini
wakati wa mapumziko, nimepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa
Simba kuhusiana na mwenendo wa timu kwa hivi sasa.
“Kwa sasa
namaliza majukumu yangu kikazi halafu nitarudi tena safari nyingine nchini kwa
ajili ya kuendelea na mazungumzo na viongozi wenzangu wa Simba ili tujue
tunaweza kufanya nini kuendelea kurekebisha mambo,” alisema.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Malkia wa Nyuki
alisindikizwa na mwanaye Fatma, maarufu kama Nyuki Mtoto na watu wengine
wawili.
Baada tu ya
yeye kupanda ngazi za ndege hiyo, walinzi na wafanyakazi waliokuwa nje ya ndege
hiyo nao waliingia na ikaanza safari kwenda Comoro.
| AKIANZA KULIKWEA DEGE HILO |
| DEGE LENYEWE, FAST JET CHAMTOTO.. |







0 COMMENTS:
Post a Comment