Kocha
Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amelalamika kwamba joto kali linampa wakati
mgumu.
Logarusic
amesema kiwango cha nyuzijoto hadi zaidi ya 30 kinamchanganya kutokana na
mazingira aliyokuwa anaishi.
“Kwetu
Croatia kiwango cha baridi ni kikali kwa kipindi hiki, kipo hadi chini ya tano
(-5C).
“Sasa
hapa joto ni juu ya thelathini, si kitu kidogo nakuambia. Nachanganyikiwa na
ninalazimika kunywa maji mengi sana.
“Lakini
sina ujanja, ndiyo kazini kwangu na nitalazimika kuendelea hadi nitakapozoea,”
alisema.
Pamoja
na kujitahidi, lakini Logarusic amelazimika mara nyingi kunywa maji au kutumia
jezi yake kufuta jasho usoni mwake.
0 COMMENTS:
Post a Comment