Uongozi
wa Simba chini ya kamati ya utendaji umekubali kumpa mkataba mpya wa kocha
msaidizi, Selemani Matola.
Habari
kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Matola alifanya mazungumzo jana na uongozi wa
Simba kujadili suala hilo.
“Wamezungumza
jana na ikiwezekana leo au kesho Matola anaweza kumaliza kila kitu kwa kusaini
mkataba,” kilieleza chanzo.
Awali,
Kocha mpya wa Simba, Logarusic alionekana kuchukizwa na Matola kutoonekana
mazoezini.
Lakini
baadaye alielezwa kuwa anasubiri kuingia makubaliano kwanza na uongozi wa Simba
kwa kuwa hakuwa na mkataba.
Matola
ameanza kazi jana baada ya makubaliano hayo na uongozi.
0 COMMENTS:
Post a Comment