Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe amesema hatakubali kukatwa mshahara wake
na kocha mpya wa klabu hiyo, Mcroatia, Zdravok Logarusic, baada ya kuchelewa
kujiunga na wenzake mazoezini.
Hivi
karibuni kocha huyo wa Simba alidai kuwa atawakata mishahara wachezaji wote
waliochelewa kuripoti mazoezini bila kutoa taarifa.
Tambwe
amesema kuwa, wakati akiondoka Bongo, aliambiwa atapewa taarifa ya lini
wataanza kambi lakini hadi mazoezi yameanza hajapata taarifa yoyote.
“Mimi
siwezi kukubali kwa kuwa hawajatupa taarifa kama wameanza mazoezi, tunasubiri
mpaka watupe taarifa wao wenyewe,” alisema Tambwe ambaye yupo nchini Burundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment