Yanga imemalizana na Charles
Boniface Mkwasa katika nafasi ya kocha msaidizi na ndiye ataongozana na timu
hiyo kwenda kambini barani Ulaya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga
zimeeleza Mkwasa ataondoka na timu hiyo kwenda Ulaya itakapokwenda kuweka
kambi.
“Yanga itaweka kambi barani Ulaya
kujiandaa na Ligi Kuu Bara. Kwa kuwa haina kocha mkuu, Mkwasa ndiye ataongoza
msafara.
“Unajua makocha wawili walikuwa
wanapewa nafasi, (Juma) Mwambusi na Mkwasa lakini inaonekana kocha huyo mkongwe
amepewa nafasi,” kilifafanua chanzo hicho.
Mkwasa amewahi kuichezea na kuifundisha
Yanga kwa vipindi tofauti.
Juhudi za kumpata jana baada ya kupata
taarifa hii ziligonga mwamba kwa kuwa simu yake ilikuwa inaita tu bila
kupokelewa.
Lakini juzi alinukuliwa na vyombo
mbalimbali vya habari akisema amefanya mazungumzo na Yanga na vingine vilisema
walishamalizana.
Yanga imeamua kufanya mabadiliko katika
benchi la ufundi baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba katika mechi ya kirafiki
ya Nani Mtani Jembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment