March 29, 2014


Kama kikosi cha Al Markhiya kitafanikiwa kushinda mechi zake mbili zilizobaki basi moja kwa moja kitapanda hadi Ligi Kuu nchini Qatar.
Kiungo Mtanzania wa Al Markhiya, Mwinyi Kazimoto ameliambia Championi Jumamosi kuwa kesho Jumapili ndiyo fainali kwao.
“Kesho tunacheza mechi moja kati ya hizo mbili za mwisho ambazo tunatakiwa kushinda ili tupande daraja na itakuwa mechi ngumu sana,” alisema Kazimoto, kiungo wa zamani wa Simba.
“Unajua ugumu unatokana na hivi, tunakutana na timu inaitwa Shahania na ndiyo tunagombea nao nafasi ya kushinda, wao wakishinda mbili zilizobaki pia wanapanda.
“Shahania wana pointi 27 na sisi tuna 25. Hivyo tukiwafunga tunawaondoa kwenye reli na tunakwenda kushinda mechi ya mwisho, basi tumepanda. Lakini wakitufunga, nafasi inakuwa ya kwao.”
Kazimoto ameonyesha uwezo mkubwa na amekuwa tegemeo katika kikosi cha Al Markhiya tokea alipojiunga nacho akitokea Simba.

Kocha wa kikosi hicho amekuwa akimuamini na kumchezesha namba nane kwa ajili ya kuichezesha timu yake hiyo ambayo msimu huu imekuwa na mafanikio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic