March 29, 2014


Kocha Mpya wa kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ameanza kazi yake hiyo akiwa bado nyumbani kwao Uholanzi barani Ulaya.
Martinnus Ignatius Nooij ametuma programu kwa ajili ya
kuwaendeleza vijana wa kikosi cha Taifa Stars kinachojengwa ambacho kimeweka kambi mjini Tukuyu.
Mart amewahi kuinoa timu ya taifa chini ya miaka 20 ya Burkina Faso na kubwa ya Msumbuji na ndiyo amekuwa chaguo la kwanza la TFF.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, zinasema Nooij maarufu kama ‘Mart’ ametuma programu ambayo wanatumia vijana hao.
“Kocha ametuma programu maalum ya wiki mbili na vijana chini ya benchi la ufundi ambalo liko nao mjini Tukuyu wamekuwa wakiifuata.
“Kocha mwenye ameishatumiwa picha kuhusiana na vijana hao na anajua mambo mengi sana ambayo yanaendelea, unaweza kusema yuko pamoja na nasi,” kilieleza chanzo.

Kocha huyo anatarajia kutua nchini hivi karibuni kuchukua nafasi iliyoachwa na Kim Poulsen raia wa Denmark baada ya TFF kuamua kuvunja naye mkataba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic