March 9, 2014



Na Saleh Ally, Alexandria
Hali ya hewa ya jiji la Alexandria imeonekana kuwa tofauti kidogo na ile ya jiji la Cairo.


Baridi imekuwa kali kiasi ukilinganisha na ile ya Cairo na kuwapa wakati mgumu wachezaji wa Yanga.

Hata hivyo, baadhi yao wamesema wanaweza kupambana licha ya baridi kuwa kali dhidi ya Al Ahly na kuimaliza.

Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kucheza hatua ya 16 Bora inapigwa leo kwenye Uwanja wa Max jijini hapa.

Katika mechi ya kwanza, Yanga ilishinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kabla ya mechi kuhamishiwa jijini hapa, ilipangwa kuchezwa Cairo ambako hakukuwa na baridi kali kama ilivyo hapa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic