Kiungo mkongwe wa Simba, Amri
Kiemba, yupo katika wakati mgumu kutokana na
kumpoteza baba yake mzazi mzee Athuman Kiemba, jana
Ijumaa.
Kiemba amesema kuwa baba yake ambaye alikuwa Sumbawanga, Rukwa amefariki dunia baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Kiemba aambaye alikuwa akizungumza huku akionyesha kuwa na majonzi, alisema kuwa marehemu baba yake mbali ya
kuwa ni mzazi wake lakini alikuwa ni rafiki yake mkubwa na alikuwa akimtegemea
katika masuala mbalimbali binafsi na ya kikazi yaliyomhusu.
“Nimeondokewa na baba leo (jana) asubuhi, aliugua kwa muda mrefu,
inaniuma kwa kuwa alikuwa ni kama rafiki na mshauri wangu hasa kwenye mambo ya
kifamilia.
“Mpaka sasa bado nipo Dar nafuatilia usafiri ili niwahi eneo la tukio
kwa ajili ya mazishi ya mzee wetu,” alisema Kiemba.
SALEHJEMBE INAMPA POLE KIEMBA PAMOJA NA FAMILIA YAKE KUTOKANA NA MSIBA HUO MZITO.
MWENYEZI MUNGU AMPUNGUZIE ADHABU ZA KABURI NA AHELA.
0 COMMENTS:
Post a Comment