March 27, 2014





Kweli matatizo huandamana! Siku chache tu baada ya kuumia na kusafirishwa nje ya Hispania kwa ajili ya matibabu, mchezaji Jese Rodriguez amepata balaa tena.

Nyumba ya Jese iliyo katika eneo la La La Finca ndani ya kitongoji cha Pozuelo de Alarcón jijini Madrid imeungua moto.


Jese bado yuko hospitali akiendelea na matibabu lakini walinzi watatu wa eneo hilo walifanya kasi ya ziada kuuziba moto huo na inaelezwa asilimia 15 ilikuwa imeishateketea.
Inaelezwa Jese ndiyo alikuwa na siku 30 tokea aikodi nyumba hiyo na sasa imeungua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic