Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameonyesha ukomavu katika uongozi wa soka baada ya
kukataa wachezaji wake kuuzwa katika kipindi timu yao inapambana kutetea
ubingwa wa Tanzania Bara.
Manji
amekataa kuuzwa kwa Emmanuel Okwi kwa klabu ya Al Ain ya Abu Dhabi ambayo
ilikuwa tayari kutoa kitita cha dola 500,000 kwa kuwa si wakati
mwafaka.
Lakini
akasisitiza hata Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hawezi kuondoka wakati Yanga ikiwa
inapambana katika wakati mgumu.
Chanzo cha
uhakika kutoka ndani ya Yanga kimeeleza, Manji amesisitiza kuwa kama mchezaji
anauzwa, lazima kuwe na uhakika wa yule atakayeziba pengo lake kama yuko ndani
ya timu au atakayenunuliwa.
“Unajua
wale jamaa hawakuwa wamekuja official (kiofisi) kabisa Yanga kumtaka Okwi,
lakini taarifa zilishaufikia uongozi na mwisho mwenyekiti alisikia.
“Baada ya
hapo akasisitiza hakutakuwa na mchezaji atakayeondoka katika kipindi Yanga
inapambana kuwania ubingwa. Badala yake akataka kuwe na utataribu mzuri wa kuwauza
wachezaji na si kuangalia fedha tu,” kilieleza chanzo.
“Lakini
kuhusu Cannavaro pia amesema huu si wakati mzuri na tuna mechi muhimu za
kumaliza ligi, hivyo tufanye mambo kitaalamu.”
Al Ain
ambayo anachezea Asamoah Gyan raia wa Ghana, imeonyesha kuvutiwa na Okwi tokea
akiwa Etoile du Sahel ya Tunisia, lakini ikawa inachanganywa na mgogoro wake.
Wakati Al
Ahly ilivutiwa na Cannavaro wakati Yanga ilipocheza nayo mechi mbili za Ligi ya
Mabingwa Afrika na nahodha huyo wa Yanga akafunga mechi zote mbili.
Championi
Jumamosi lilifanya juhudi za kumsaka Manji na kupata ufafanuzi kuhusiana na
suala hilo la kuzuia wachezaji kuuzwa.
“Si kuzuia
kwa nia mbaya, lakini Yanga inapouza wachezaji lazima iwe na uhakika kama ina
muda wa kuwaongeza na nani anaongezwa. Huwezi kuuza mchezaji halafu wewe
ukabaki dhaifu, si sahihi,” alisema kwa ufupi na kusisitiza viongozi wengi hasa
watendaji wanaweza kulizungumzia.
Msimu uliopita, Simba
ilimuuza Okwi bure kwa Etoile du Sahel wakati ikiwa katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, hali iliyosababisha kuzorotesha kikosi hicho ambacho
kilitolewa kwa aibu ya kufungwa jumla ya mabao 6-1 baada ya kufunga bao 1-0
jijini Dar na 5-1 ugenini Angola
0 COMMENTS:
Post a Comment