March 29, 2014

NYUMBA YAO, INAPOJENGWA HOSPITALI HIYO

Familia ya dereva nguli na maaufu zaidi duniani wa magari ya formula 1 au langalanga, Michael Schumacher imeamua kutumia pauni milioni 10 kujenga hospitali.


Hospitali hiyo itajengwa kwenye jumba la kifahari linalomilikiwa na familia hiyo ambalo liko katika eneo la Ziwa Geneva.
Mke wa Schumacher  ambaye sasa amefikisha miezi mitatu kamili tokea alipolazwa akiwa hospitali baada ya kuteleza na kuanguka halafu akagonga jiwe ndiye aliyeshukua uamuzi huo.
SCHUMACHER AKITELEZA KWENYE BARAFU

CORINNA AKIWA NA MUMEWE

Corinna Schumacher, 45, amechukua uamuzi huo akianza na kutoa pauni milioni 500 kuanza kazi hiyo katika jumla lao la kifahari ambalo linagharimu pauni milioni 25 kwenye uso wa Ziwa Geneva nchini Switzerland.
Imeelezwa uamuzi huo unatokana na ripoti ya madaktari katika hospitali aliyolazwa nchini Ufaransa kusema ni asilimia chache sana zinaonyesha Schumacher ataamka tena.
HOSPITALI ALIYOLAZWA SASA NCHINI UFARANSA

Kutokana na hali hiyo, ameona ni lahisi kuwa karibu na mumewe akiwa nyumbani kwa kuwa kila siku husafiri zaidi ya kilomita 150 kwenda na kurudi hospitali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic