Baada ya ukimya na utata, sasa
imetangazwa kuwa mechi kati ya mabingwa Afrika, Al Ahly na wale wa Tanzania
Bara, Yanga itapigwa kwenye Uwanja wa Max mjini Alexandria.
Mji huo uko kwenye pwani ya bahari ya Mediterranean,
kilomita zaidi ya 200 kutoka katika jiji hili la Cairo, mwendo wa zaidi ya
masaa mawili.
Awali ilikuwa siri, lakini leo mchana kiongozi wa umoja wa klabu za Misri, Tharwat Swelam
ameviambia vyombo vya habari mechi hiyo itapigwa bila ya mashabiki.
“Lakini muda utakuwa ni saa moja usiku
(saa mbili Bongo) kama ilivyopangwa awali, pia hatutaruhusu mashabiki,”
alisema.
Kutokana na uamuzi huo, Yanga sasa
inalazimika kusafiri tena kwenda Alexandria nab ado uongozi wake haujatoa
msimamo wake.
Awali uongozi wa Yanga ulisema kama
mechi itachezwa Alexandria basi lazima wapewe ndege, lakini mchana huu uongozi
wa Al Ahly umeliambia Championi Ijumaa kuwa bado uko katika sheria za Caf..
“Mechi ikibadilishwa baada ya siku tatu
kabla ya siku iliyopangwa hakuna tatizo kwa sheria za Caf na pake Alexandiria
si mbali,” alisema Mohamed Mowad ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya habari.
Suala hilo lilikuwa na utata mkubwa,
lakini mwisho limefikia hapo na ainaonekana Al Ahly wana hofu ya kufanyiwa fujo
na mashabiki wao iwapo watapoteza mchezo huo.
Lakini Watanzania wanaoishi hapa
wanasema hizo ni mbinu za kuwavuruga Yanga ili wazidi kuchanganyikiwa.
Baadaye jioni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema amepata taarifa hizo na tayari analifanyia kazi.
"Kweli tumepata taarifa hizo na tayari tumeanza kulifanyia kazi suala hilo," alisema Sanga.
SOURCE: CHAMPIONI
Hizo ni njama na figisu figisu za wapinzani tu, mwaka huu ni wa kifo cha waarabuu tu hata wafanye nini wasahaelekea kibla.....
ReplyDelete