March 22, 2014

REFA TUMAINI, AKIWA KWENYE BAJAJ YAKE KWENYE KITUO CHA BAJAJ MWENGE JIJINI DAR.

Mwamuzi maarufu kwa kazi yake ya kuendesha Bajaj, ambaye alichezesha mechi ya Mbeya City dhidi ya Rhino Rangers, Tumaini Godfrey, ameondolewa kuchezesha mechi zote za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kutokana na kutoumudu mchezo huo na kusababisha wachezaji kuchezeana rafu mbaya.


Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Machi 8, 2014 ulisababisha wachezaji kadhaa kuumia akiwemo Richard Peter ambaye alivunjwa mbavu tatu na kipa wa Rhino, hali iliyosababisha azimie uwanjani.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwalimu Nassor Said, amesema kamati hiyo imeamua kuwasimamisha waamuzi wawili ambao ni Tumaini na Ahmed Kikumbo kuchezesha mechi za ligi kuu.

Alisema wamefikia kutoa maamuzi hayo baada ya kupitia ripoti za kamishna wa mchezo huo.

“Mwamuzi Tumaini Godfrey hakuwa makini baada ya mchezaji wa Mbeya kufanyiwa rafu na kuumizwa, yeye hakuchua hatua yoyote na aliweza kulifumbia macho tatizo hilo.


“Ahmed Kikumbo yeye ilikuwa katika mchezo wa Rhino na Ashanti United, alifanya kosa la kumpa mchezaji wa Ashanti kadi nyekundu ambayo haikustahili, alijitetea kwa kusema alijisahau na kudhani mara ya kwanza alimpatia kadi ya njano,” alisema Nassoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic