TAMBWE KAZINI |
Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe na beki wa kati, Donald Musoti, wametamba kuwa lazima
wawakalishe Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Bara, keshokutwa Jumapili
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hizo zinakutana ambapo Simba ina pointi 36 na ikiwa inashika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, huku Coastal ikiwa nafasi ya saba ikiwa
na pointi 26.
Tambwe amesema kuwa hana hofu na beki wa Coastal, Juma Nyosso kwa kuwa
anaamini ni beki wa kawaida kwake.
“Nimejipanga vizuri, sina hofu na Nyosso, kwanza ni wa kawaida
hanitishi kwa lolote, ninajiamini kuwa nina uwezo wa kuisaidia
timu yangu kupata ushindi.”
Upande wa Musoti, raia wa Kenya, alisema anaamini Simba
ipo sawa na haoni kinachoweza kuzuia ushindi wao katika mechi hiyo. “Tupo
tayari na ‘gemu’ hiyo na hakuna wa kuhofia, labda kilichosubiriwa ni siku ya
kukutana,” alisema Musoti.
0 COMMENTS:
Post a Comment