March 8, 2014

JIJI LA ALEXANDRIA
Na Saleh Ally, Alexandria
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wametua salama kwenye mji wa Alexandria nchini Misri.

Yanga imetua katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Misri na kufikia katika Hoteli ya Sheraton Montazah ambayo inatazama ufukwa wa bahari ya Mediterranean.
HOTELI YA SHERATON WALIYOFIKIA

Yanga ilisafiri kwa mwendo wa saa tatu katika Kilomita 220 kutoka jijini Cairo, kuja hapa kwa ajili ya mechi yao itakayopigwa kesho usiku kwenye Uwanja wa Max.

Tayari mabingwa watetezi, Al Ahly pia imewasili jijini hapa kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kufuzu hatua ya 16 Bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic