April 26, 2014


Bendera zote katika eneo la Uwanja wa Camp Noun a ile shule maarufu ya soka ya La Masia, zinapepea nusu mlingoti.

Hiyo ni dalili ya heshima kwa kocha Tito Vilanova ambaye amefariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 45 kutokana na ugonjwa wa kansa.
Vilanova ambaye misimu miwili iliyopita alijibu mapigo kazi ya Jose Mourinho kwa kuchukua ubingwa wa Hispania akiwa na pointi 100, amepambana na ugonjwa wa kansa hadi mwisho wa maisha yake.

Baadhi ya ujumbe ulionezwa katika sehemu mbalimbali za jiji la Barcelona ni kumpongeza kutokana na juhudi zake za kupambana na kansa hadi mwisho na baadaye kumtakia kupumzika kwa amani kama shujaa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic