April 26, 2014

AMROUCHE
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya, Adel Amrouche anatarajia kutua leo jioni jijini Dar es Salaam kuiunga mkono timu ya taifa ya vijana ya Kenya ambayo iko jijini humo.

Timu ya taifa ya Kenya ya vijana chini ya miaka 20 iko jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi yake ya kesho dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.
..AKIWA NA WANYAMA.
Timu huyo zitacheza kesho mechi ya kuwania kucheza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika la vijana.
Katika mechi ya kwanza mjini Machakos, Kenya, timu hizo zilitoka suluhu.
..AKIWA NA STEVEN KESHI WA NIGERIA
Hivyo sare yoyote itaifanya Kenya kusonga mbele na Tanzania inachotakiwa ni kushinda tu.
Akizungumza kutoka Nairobi, Amrouche raia wa Belgium kwenye asili ya Algeria alisema kawaida amekuwa karibu na timu za vijana.

“Nawaunaga mkono, nataka kuona wanafanya vizuri na hili ni sehemu ya jukumu langu,” alisema kocha huyo aliyeipa Kenya ubingwa wa Kombe la Chalenji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic