April 26, 2014


Aibu nyingine, Taifa Stars imefungwa katika mechi ya kirafiki kwa mabao 3-0 na wageni wake Burundi katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao mawili ya Burundi yamefungwa na washambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe na yule wa Yanga, Didier Kavumbagu.
Bao la tatu lilifungwa na Hamad Ndikumana umbali wa karibu mita 45 na kumuacha kipa Deogratius Munish ‘Dida’ akiwa hajui la kufanya.
Mashabiki waliokuwa uwanjani hapo walionyesha kutofurahishwa na hali hiyo na kuanza kuwazomea wachezaji hasa wale kutoka katika kikosi cha maboresho cha Taifa Stars ambao walianza watano katika kikosi cha kwanza.
Baadaye mashabiki hao walimzomea kocha Salum Mayanga wa Taifa Stars wakati akiingia vyumbani wakati wa mapumziko na baadaye alipokuwa kwenye benchi.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic