MANCHESTER CITY |
Na Saleh Ally
UTAMU upo kesho, hakuna
anayeweza kukataa tena kwamba Ligi Kuu England, maarufu kama Premiership
imekuwa tamu mpaka basi.
Bingwa wa ligi hiyo
atapatikana kesho, ndiyo siku ya mwisho ya ligi hiyo na hili linalonyesha ubora
wake na namna mambo yalivyo magumu.
Iwapo utaamua runinga
kubwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kualika mashabiki, bila
shaka watu watafikia nusu au kuujaza kabisa hasa wakikubali kukusanyika na
kuangalia pamoja mechi za mwisho za Premiership ambayo ni maarufu zaidi duniani
katika soka.
Majibu ya walioteremka
daraja yameishapatikana, Cardiff City, Fulham na Norwich City wanajua kabisa kuwa msimu ujao watakipiga
Ligi Daraja la Kwanza England.
LIVERPOOL |
Ukiangalia kwenye
msimamo, inaonekana hivi, kama Wes Brom yenye pointi 36 itapoteza mechi ya
mwisho itabaki ilipo na kama Norwich atashinda, atafikisha 36 pia lakini
tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa inamuangusha kwa kuwa lazima ashinde
zaidi ya mabao 15, haitawezekana.
Ukirudi kwenye ubingwa
sasa hakuna ubishi tena kwamba Chelsea ilishajiondoa kaika mbio hizo hasa baada
ya ile sare ‘tasa’ dhidi ya Norwich na kuifanya ifikishe pointi 79 ambazo hazina faida tena.
Ikishinda ina uwezo wa
kufikisha pointi 82 wakati Manchester City imeishafikisha 83. Maana yake haimo
na kwenye kuuwania ubingwa kesho, Jose Mourinho analitambua hilo.
Manchester City ndiyo
wenye nafasi kubwa zaidi lakini bado nafasi hiyo unaweza kuiweka kwa Liverpool
kwa kuwa huu ni mchezo soka.
Man City:
Ndiyo timu yenye nafasi
kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa kuwa ushindi na hata
sare, bado mambo yanaweza kuwa mazuri kwa vijana wa Manuel Pellegrini.
Iwapo itashinda, hata
kama ni bao moja tu, basi muhimu pointi tatu na itakuwa na 86 ambazo haziwezi
kuguswa na timu yoyote msimu huu.
Hata kama itatoka sare
bado ikiwa na pointi 84 ambazo Liverpool atazifikia kama akishinda, lakini bado
tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ya City iko juu, imefunga mabao 100 na
kufungwa 37 tu.
Ugumu kwa Man City, hata
kama ina kiwango kizuri inakutana na West Ham ambayo haina presha hata kidogo
na wala si timu ya kuidharau.
West Ham jina la utani
kama ‘Wagonga Nyundo’, ina pointi 40 katika nafasi ya 12. Hata ikishinda
itabaki hapo ilipo kwa kuwa Crystal Palace kwenye nafasi ya 11 ina pointi 44.
Maana yake, West Ham
itacheza mechi hiyo bila ya presha na inachoangalia ni rekodi au kuepuka kuwa
daraja la Man City kutwaa ubingwa.
Liverpool:
Baada ya kuteleza na
kuruhusu mabao matatu kusawazishwa dhidi ya Crystal Palace na kuzaa sare ya bao
3-3, kuifanya iwe haina ujanja na kwake kikubwa ni ushindi tu katika mechi yake
ya mwisho dhidi ya Newcastle ikiwa nyumbani Anfield, kesh.
Pamoja na kushinda,
Liverpool watalazimika kupiga magoti kabla na wakati mechi ikiendelea ili
kuwaombea Man City ‘dua mbaya ili wapoteze mechi yao dhidi ya West Ham wakiwa
kwao Etihad.
Iwapo wao watashinda na
kufikisha pointi 84, halafu City wakapoteza maana yake kombe ni lao, sasa
inategemea watazifanyaje kazi hizo mbili za kusaka ushindi na ‘maombi’.
Lakini tatizo kwao
linaweza kuwa hivi, pamoja na mashabiki wa Newcastle lakini hata ikipoteza
haitashuka au ikishinda haitapata lolote muhimu.
Newcastle ina pointi 49
katika nafasi ya tisa, iwapo itashinda itakuwa na pointi 52, wakati Southampton
katika nafasi ya nane ina pointi 55 tayari.
Hivyo Newcastle itakuwa
kwenye nafasi nzuri kwa kuwa itacheza mechi hiyo bila ya kuwa na presha hata
kidogo.
Unapocheza na kikosi
kisichokuwa na presha pia ni tatizo, kwani wao wanakuwa katika nafasi nzuri ya
kufanya mambo kwa uhakika kuliko wewe uliyepania zaidi.
Hivyo Liverpool na Man
City pia wanapaswa kuwa makini, lasivyo, ndoto zao zinaweza kukwama katika siku
ya mwisho kabisa ya ligi.
Mechi za zote za kesho
zitakuwa tamu, lakini mbili za mjini Manchester na ile ya jijini Liverpool
ndiyo zitakuwa tamu zaidi kwa kuwa zina majibu ya nani mfalme mpya wa England
baada ya yule wa msimu uliopita Man United, kujiondoa mapemaaaa!!
0 COMMENTS:
Post a Comment