Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos amejaaliwa kupata mtoto wake wa kwanza
na amempa jina la Sergio.
Mpenzi wake, Pilar Rubio amejifungua mtoto wake huyo wa kiume leo na Ramos
amethibitisha hilo.
“Pilar na mimi tuna furaha kubwa kuwaambia tumefanikiwa kupata mtoto wa
kiume na wote, yeye na mama yake wako katika afya njema,” alisema Ramos.
Sergio amezaliwa jana saa 1:43 usiku akiwa na kilo 3.2 na familia hiyo ya
beki huyo kisiki imempokea kwa furaha kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment