SIMEONE |
Kocha Mkuu wa Atlético de Madrid, Diego
Simeone amesema kikosi chake kitambana hadi mwisho wa La Liga.
Simeone amesema anaamini wana nafasi
lakini majibu ya kila watakachokifanya yatapatikana kutokana na matokeo mazuri.
Akiizungumzia mechi yao dhidi ya Malaga,
kesho, Simeone amesema: ”Nimekuwa nafikiria mengi kuhusiana na kipindi hiki.
“Tunacheza na timu ambayo haina hofu ya
kuteremka na ina wachezaji wazuri sana hivyo si lahisi lakini tutapambana hadi
mwisho.”
Atletico ina nafasi ya kutwaa ubingwa kama
ilivyo kwa Barcelona na Real Madrid.
Kila moja imebakiza mechi mbili na kila
moja itacheza mechi moja kesho usiku.
Pamoja na hivyo timu hiyo imeingia fainali
ya Ligi ya Mabingwa na itacheza na wapinzani wake wakubwa, Real Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment