ZUTTA |
Pamoja na kuondoka, kwenda nchinI Saudi Arabia, Kocha Hans van Der Pluijm ameanza mazungumzo na kiungo, Joseph Tetteh Zutah wa Medeama SC ya Ghana kuziba pengo lililoachwa na Frank Domayo.
Kabla ya
kuchukua uamuzi wa kuondoka Yanga na kujiunga na Shoala SC ya Saudi Arabia tayari
Pluijm alimpendekeza Zutta kuchukua nafasi ya Domayo ambaye alisisitiza amekuwa
havutiwi na uchezaji wake.
Championi
Jumamosi limenasa mazungumzo kati ya wakala kutoka Ghana aitwaye Richard
wakiwasiliana kuhusiana na kiungo huyo.
Pluijm
amemueleza Richard kwamba atawasili nchini Ghana baada ya siku chache kwa ajili
ya kutafuta wachezaji wawili kwa ajili ya Yanga ambao ni mshambuliaji na kiungo
mkabaji.
Kuhusiana
na kiungo huyo, Pluijm ametoa sifa zake ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukaba,
kumiliki mpira na kupambana vilivyo mambo yanapochafuka, yaani wanapokuwa
wamezidiwa.
Lakini
kwenye ujumbe huo mfupi, Pluijm akamtaja Zutta kuwa ndiye chaguo lake na hivyo
apewe taarifa kuhusiana na ujio wa Mholanzi huyo aliyewahi kuwa kocha wake.
“Habari
yako Richard, mimi ni Kocha Hans van der Pluijm, nataka wachezaji wawili kutoka
Ghana, mshambuliaji na kiungo mwenye uwezo wa kupambana, kukaba na kuichezesha
timu.
“Najua
Joseph Zutah atafaa, hivyo muambie nia yangu pamoja nia yangu ya kumleta Yanga,
asiwe na hofu kwa kuwa msimu ujao watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho,”
ilieleza sehemu ya ujumbe huo.
Pluijm
ameondoka nchini jana na leo alitarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja
kuifudisha Shaola ya Saudi Arabia ambayo itakuwa ikimlipa dola 20,000 kwa
mwezi.
Lakini
ameahidi kuisaidia Yanga kupata mshambuliaji mmoja na kiungo ambaye
alipendekeza atafutwe hata kabla ya Domayo kujiunga na Azam FC kwa kitita cha
Sh milioni 70.
Pamoja
na kuifundisha Berekum Chelsea kwa mafanikio, Pluijm ambaye ameoa mke raia wa
Ghana aliwahi kuifundisha Madeama na Zutta ni kati ya wachezaji aliowanoa
wakati akiwa kocha nchi Ghana.
SOURCE`; CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment