June 28, 2014


DALALI (KULIA) AKIWA NA AVEVA


Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali leo ameonyesha ukomavu mkubwa baada ya kutaka makundi ndani ya Simba yavunjike.
Uchaguzi unafanyika kesho jijini Dar es Salaam na wanachama wa Simba wametakiwa kujitokeza kwa wingi.
Dalali amewataka wanachama wote wa Simba kuungana na kuachana na masuala ya uchaguzi.
Kabla ya kuanza kufunguka, Dalali aliwataka wanachama kuacha kumpakazia Evans Aveva kwamba aliuza gari.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akimsindikiza mgombea anayemuunga mkono, Evans Aveva, Dalali alisema:
“Simba lazima iungane, hatuwezi kusema eti kuna makundi wakati lengo ni kuleta maendeleo.

“Kama tutataka maendeleo, halafu tutakuwa na makundi, basi haina faida ya kupata vingozi bora.
“Lazima tuungane na kuifanya Simba iwe moja ili kuleta maendeleo.

“Simba haijawa bingwa miaka mitatu sasa, si kitu kizuri na kutokuwa na umoja ndiyo lilikuwa tatizo kubwa,” alisema Dalali.
Dalali ni kati ya viongozi vipenzi vya Wanasimba kutokana na kuwa kiongozi imara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic