June 28, 2014



Dogo mmoja Mbrazil alizamia katika chumba cha nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo.
Yago Leal, 15, aliingia chumbani kwa Ronaldo katika hoteli waliyofikia Ureno, dakika dakika chache kabla ya kuivaa Ghana. Katika mechi hiyo, Ureno ilishinda 2-1 lakini ikatupwa nje.

Yago alijificha chumbani humo baada ya kupitia dalini, baada ya Ronaldo kuwasili alimkuta na kushituka.
Lakini baada ya kujieleza, alimshusha kutoka kwenye dali, walizungumza, wakapiga picha pamoha.

"Nilijua hawezi kuwaita walinzi, pia nilimuomba asifanye hivyo. Alikuwa mtu poa sana licha ya kwamba nilikosea.

“Baada ya hapo, tulipiga picha pamoja, wachezaji wengine kadhaa pia walipiga picha na mimi, halafu nikaondoka hotelini pale kwa amani,” alisema Yago ambaye pia alijisifia kulala kitandani kwa Ronaldo kabla yeye hajaingia chumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic