June 28, 2014



Liverpool sasa iko tayari kumuuza mshambuliaji wake Luis Suarez kwa Barcelona.
Barcelona imetoa ofa ya pauni milioni 80 kumnasa mkali huyo, uhamisho huo ni kama ule Real Madrid waliotoa kumpata Cristiano Ronaldo kutoka Man United.
Inaonekana Liverpool ambayo ilikuwa haitaki kumuuza Suarez imelazimika kufanya hivyo kwa vitu viwili.
Kwanza, fedha nyingi za uhamisho ambazo ni kitita kizuri halafu majanga yasiyoisha ya Suarez ambaye ndiye mchezaji anaongoza kuwauma wenzake uwanjani kuliko mwingine yoyote tokea soka ianze kuchezwa.
Sasa Suarez anatumikia adhabu ya miezi minne na mechi 9 za kimataifa kutoka Fifa kutokana na kumuuma beki Giorgio Chiellini wa Italia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic