June 23, 2014

HANS POPE


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope, amemtamka aliyekuwa mgombea wa urais wa klabu hiyo, Michael Wambura kusema jambo kuhusiana na wanachama waliokwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi.

Hans Pope amesema waliokwenda mahakamni kufungua kesi hawawezi kutokuwa na uhusiano na Wambura.
“Kama Wambura ataendelea kukaa kimya huku akijua kuna watu wamefungua kesi mahakamani, maana yake kuna jambo.
WAMBURA

“Avunje ukimya, aseme jambo kuhusiana na suala hilo. Kama ataendelea kukaa kimya maana yake atajichafua.
“Naona si sahihi na wote tunajua haitakiwi kupeleka masula ya soka mahakamani,” alisema Hans Pope.
Tayari Hans Pope na kamati yake wameanza taratibu za usajili baada ya kamati ya rufaa ya TFF kuthibitisha kuwa Wambura aliyeng’olewa kwenye uchaguzi ya Simba, kweli alifanya kampeni kabla ya muda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic