June 26, 2014



MOJA YA MAGARI BAADA YA SHAMBULIZI LA JANA.

Pamoja na kikosi chake kufanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia, Kocha wa Nigeria, Steven Keshi ameonekana kutokuwa na furaha.
Bila ya woga, Keshi ameeleza kuwa ameshangazwa na mashambulizi yanayoangamiza mashabiki wa soka nchini mwake na kusisitiza kuwa wanachofanya memba wa kundi la Boko Haram si jambo sahihi.
Shambulizi la mwisho ni jana wakati Nigeria ilipofungwa mabao 3-2 na Argentina, lakini ikasonga mbele.
KESHI
Watu 16 wameuwawa katika shambulizi hilo la bomu jijini Abuja.
“Sielewi wanafanya nini hawa watu, hawajui wanauwa watu wasiokuwa na hatia,” alihoji Keshi.
Kabla ya mechi hiyo, wakati Nigeria ikicheza mechi dhidi ya Iran, pia walifanya shambulizi na kuuwa watu 14.
Mashabiki wa Nigeria wamekuwa wakilaani mashambulizi hayo ya Boko Haram waliojichimbia Kaskazini mwa nchi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic