June 27, 2014



Kocha mpya wa Yanga, Marcio Maximo amewataka wadau kuvuta subira katika mambo atakayoanza kufanya kwa kuwa soka yanahitaji subira.
“Mambo ya soka yanataka kwenda taratibu na wakati mwingine haraka, lakini sidhani kama itakuwa vizuri kwenda harakaharaka.
“Ndiyo maana sikutaka kuzungumza hadi kutakapokuwa na mkutano wa waandishi, baadaye nitaanza kazi.
“Hivyo waambie watu wote, Wanayanga, waandishi na wengine wawe na subira kwa kuwa niko Yanga sasa kwa miaka miwili,” alisema Maximo.
Maximo ametua Yanga ambayo ameingia nayo mkataba wa kuinoa kwa miaka miwili sambamba na msaidizi wake Leonardo Leiva Martins.
Maximo anatarajia kuwa na mkutano na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic