June 28, 2014



Pamoja na kukumbana na adhabu kubwa baada ya kumuuma beki Goirgio Cheillini wa Italia, Luis Suarez amepokelewa kama shujaa kwao Uruguay.
Ajabu, hata Rais wa Uruguay, Jose Mujica akiwa katika safari zake alimsubiri Suarez na kumsalimia uwanja wa ndege.


Baada ya mshambuliaji huyo kuwasili na kwenda nyumbani kwake, mashabiki kibao walijitokeza.
Walikwenda kwenye nyumba yake kwenye jiji la Montevideo na kuanza kuimba nyimbo za kumsifia hadi alipotoka na kuwapungua mkono akiwa amewabeba waanaye wawili.
Suarez hakuonyesha kuwa na hofu hata kidogo, badala yake aliwapungia mkono kwa raha zake.
Hali hiyo inaonyesha Waruguay wanavyojivunia upuuzi wa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 ambaye amekuwa bingwa wa kuwang’ata wachezaji wenzake.
Fifa imemgungia miezi minne, mechi 9 za kimataifa akiwa na Uruguay pamoja na faini ya pauni 65,000.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic