Rais wa Simba, Evans Aveva amesema ameipokea barua iliyotoka kwa
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na kuichambua kuwa ni sehemu ya mabadiliko
makubwa katika mchezo wa soka nchini.
Aveva ameiambia SALEHJEMBE kwamba, Manji amempongeza na pia
kuelezea kuhusiana na ushindani wa Simba ambao unapaswa kuwa ni uwanjani.
“Kanipongeza kuhusiana na ushindi lakini hii pia ni kwa niaba ya timu
nzima ya uongozi iliyoingia madarakani. Hili ni jambo zuri na la kizalendo na
hii ndiyo maana ya klabu zetu, Simba na Yanga, ushirikiano ni jambo jema.
“Nimepokea kwa mikono miwili pongezi za mwenyekiti wa Yanga, nasisitiza
kiuanamichezo ni jambo jema,” alisema Aveva akionyesha kujiamini.
Manji alimuandikia Aveva barua kumpongeza mara baada ya kuibuka na
ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake, Andrew Tupa.
Aveva amekuwa mwanachama wa kwanza wa Simba kushika nafasi ya rais wa
klabu hiyo lakini Manji ameweka rekodi ya kumuandikia kiongozi wa juu wa Simba
barua ya kumpongeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment