Simba sasa imeamua kuvuka mipaka, imefunga
safari hadi nchini Ivory Coast na kumshawishi kiungo Kwizera Pierre kutua
nchini na kujiunga nayo.
Kwizera ni raia wa Burundi anakipiga katika
kikosi cha Fad Abidjan pia ni kati ya viungo tegemeo wa timu ya taifa ya
Burundi.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Simba
zinaeleza Kwizera ambaye ana sifa ya kukaba sana, kupiga mashuti makali ndiye
ameonekana chaguo sahihi badala ya Jerry Santo.
“Kamati ya usajili inaendelea kufanya juhudi
za kumpata Kwizera, ikiwezekana anaweza kuwasili nchini Ijumaa kwa ajili ya
mazungumzo na mambo yakiwa safi atasaini.
“Uongozi wa juu wa Simba pia umekuwa
unafanya kazi kubwa na ushirikiano wa karibu na kamati ya usajili ikiwa ni
kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo, imeelezwa, Kwizera amekuwa na
ndoto za kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya, lakini Simba imetumia
ushawishi ili kuweza kumshawishi atue Msimbazi,” kilifafanua zaidi chanzo.
Kocha Zdravko Logarusic amekuwa akisisitiza
kupatikana kiungo mkabaji ambaye atacheza yeye au Jonas Mkude na kuifanya Simba
kuwa na uhakika katika nafasi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment