July 3, 2014

MUSLEY (MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI HIYO NA KUNDI LA FOS)


Rais wa Simba, Evans Aveva ametangaza kamati mpya ya usajili ambayo mwenyekiti wake anaendelea kubaki kuwa Zacharia Hans Poppe.
Wakati Poppe anabaki kuwa bosi, Aveva ameongeza vichwa, yaani watu wa kazi kweli ambao watashirikiana na mwenyekiti huyo kufanya kazi.
HANS POPPE.

Walioongezwa ni Kassim Dewji, Crescentius Magori na Musley Al Rawah ambao ni kati ya Friends of Simba (Fos) wakongwe kabisa na wenye uzoefu na masuala ya usajili.

Lakini bado kuna wengine wawili ambao ni Chiduo na Said Tully ambao watakuwa wakisaidiana na magwiji hao kuhakikisha usajili wa Simba unakuwa sahihi.

Baada ya kamati hizo, taarifa zinaeleza Simba inaendelea kuunda kamati mbalimbali ili kuanza kazi kwa ushirikiano na umoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic