July 3, 2014


COUTINHO AKIJIFUA NA KIKOSI CHA YANGA

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Andrey Coutinho raia wa Brazil amesema lazima atakuwa anahitaji muda.
Coutinho ameiambia SALEHJEMBE kwamba mambo yatakwenda vizuri baada ya kujifunza mambo kadhaa.
“Hapa ni mgeni, nahitaji mambo kadhaa kuzoea, then nitaanza kucheza vizuri.
“Uwanjani hakuna ugeni, ila kuna mambo kadhaa ya kuangalia na kujifunza ili kuendana na wenzako.
“Najua nitasumbuka lakini si sana, hivyo wanivumiliea niweze kuingia kwenye hali ambayo itaniwezesha kucheza vizuri,” alisema.
Raia huyo wa Brazil ameishaanza mazoezi na kikosi hicho cha Yanga kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic