July 10, 2014



Kipa Hussein Sharrif maarufu kama Casillas ameingia kwenye rekodi ya makipa wenye kiwango cha juu waliowahi kichezea Simba.

Casillas amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba na leo alisajili mbele ya katibu wa kamati ya usajili, Kassim Dewji pamoja na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na mjumbe wa kamati ya utendaji Said Tully.

Casillas aliyetokea Mtibwa Sugar atakuwa akilamba Sh 800,000 kwa mwezi.
Simba sasa itakuwa na makipa watatu ambao ni Ivo Mapunda, Casillas na Peter Manyika ambaye ni mtoto wa kipa wa zamani wa Yanga, Manyika Peter.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic