Mchezaji tenisi maarufu Maria Sharapova aliungana na
bondia nyota duniani, Floyd Mayweather katika utoaji tuzo za ESPY.
Sharapova alionekana kama ‘jitu’ kutokana na umbo lake
kubwa dhidi ya Mayweather wakati wanajitokeza pamoja jukwaani kutoa tuzo.
Tuzo hizo zilizofanyika Los Angeles, Marekani zilijumuisha
michezo mbalimbali na Ronaldo alikuwa kati ya washindi.
Staa wa Thunders, Kevin Durant ambaye anakipiga pamoja
na Hasheem Thabeet pia alikuwepo, usisahau nahodha wa Marekani, Clint Dempsey
na mwanamuziki Drake walikuwa kati ya waliohudhuria.
0 COMMENTS:
Post a Comment