July 3, 2014

CHUJI...GYM KWANZA HALAFU AKAINGIA UWANJANI.


Kiungo nyota aliyekuwa Yanga, Athumani Iddi ‘Chuji’ ameanza mazoezi leo akiwa na kikosi chake kipya cha Azam FC.

Chuji ameanza mazoezi na Azam FC kwenye Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinaeleza Chuji amesaini mkataba wa miezi sita na Azam FC.
Kabla ya kuanza mazoezi leo rasmi, Chuji alikuwa akijifua ufukweni na gym ili kujiweka sawa.

Yanga imemtema kiungo huyo katika usajili wake mpya kwa madai ya utovu wa nidhamu lakini Kocha Josep Omog wa Azam FC amemtwaa akisisitiza wachezaji wazoefu ni lulu hasa kwa michuano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic