Kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Brazil,
Andrey Coutinho, jana Alhamisi aliwakuna mashabiki waliofika kwenye mazoezi ya
timu hiyo katika Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini kutokana na kuonyesha uwezo
wa juu wa kuuchezea mpira.
Katika tukio hilo, wakati wachezaji hao
wakijifua, waligawanywa watatu kila kundi ambapo Coutinho alipangwa na mabeki
Mbuyu Twite na Juma Abdul kwa ajili ya kupiga ‘kontroo’.
Zoezi hilo lilikuwa kivutio kwa wengi na macho
mengi kuelekezwa katika kundi hilo lililokuwa na Mbrazili huyo.
Mbrazili huyo aliuchezea mpira kiufundi ambapo
alitumia viungo mbalimbali, ikiwemo mgongoni, shingoni na begani, lakini pia
Juma Abdul naye alionyesha uwezo mkubwa kwa kumjibu kiufundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment