July 4, 2014



Wakati timu ya taifa ya Brazil ikitarajiwa kuwa na kazi ya kupambana na kigingi cha Colombia kuvuka kwenda nusu fainali ya Kombe la Dunia, leo Ijumaa, Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo atawaongoza mashabiki kuishangilia timu hiyo.


Maximo, raia wa Brazil, kwa mara ya kwanza ataungana na mashabiki wa Yanga kwenye Ukumbi wa Quality Centre jijini kuishangilia timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema wamemualika kocha huyo ili kuungana na mashabiki hao wa Yanga ambao wamekuwa wakijitokeza kwenye ukumbi huo wa sinema ndani ya jengo la kibiashara la Quality Centre kushuhudia Kombe la Dunia.

“Mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi, sasa tumemwalika na kocha ili ajumuike nao kuishangilia Brazil,” alisema Njovu.

Maximo pia amesema anaamini Brazil itasonga mbele lakini haitakuwa kazi rahisi.

“Nitaungana na mashabiki wa Yanga na wapenda soka wengine tuishangilie Brazil, mechi ni ngumu kwa kuwa Colombia wana kikosi kizuri sana,” alisema Maximo.

Tangu kuanza kwa Kombe la Dunia, Yanga imetoa ofa kwa mashabiki wake kushuhudia michuano hiyo kwenye ukumbi huo ambapo mara zote Benki ya Posta ndiyo imekuwa ikidhamini na hata sasa ndiyo ambayo imemwalika Maximo.

Mashabiki wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kutokana na ukubwa wa ‘screen’ zinazotumika kuonyesha mpira, pia sauti zinazoongeza mvuto na kuwafanya waamini kama wako uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic