July 15, 2014



Uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Yusuf Manji umefanikisha zoezi ambalo litawawezesha wachezaji wa kikosi cha Yanga kuwa na nyumba zao.

Wachezaji wa Yanga pamoja na maofisa wa benchi la ufundi, watakopeshwa nyumba kupitia mishahara yao.

Yanga imefanya mazungumzo na Shirika la NSSF ambalo litawakopesha wachezaji hao nyumba zake zilizo katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizoifikia SALEHJEMBE, zimeeleza Yanga pamoja na NSSF watafanya mkutano leo kutangaza suala hilo.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji wa Yanga watakuwa wa kwanza kuingia kwenye rekodi ya kukopeshwa nyumba.
Makato ya nyumba hizo zinazoanzia Sh milioni 30 yatakuwa yanatokana na mishahara yao.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic