Wakati Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametua nchini tayari kujiunga na Taifa Stars, kiungo nyota wa Al Markhiya ya Qatar, Mwinyi Kazimoto atatua nchini kesho.
Kazimoto atatua nchini kesho tayari kujiunga na wawili hao ili kuanza kazi ya kujinoa pamoja kuisuri Stars ambayo imeweka kambi Tukuyu.
Kiungo huyo wa zamani wa Simba ambaye sasa amekubalika sana na benchi la ufundi la Al markhiya atatua nchi saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways.
0 COMMENTS:
Post a Comment