Saa 18 baada ya kutua nchini, mshambuliaji mpya wa
Yanga, Geilson Santos Santana maarufu kama Jaja ameanza mazoezi na kuwavutia
wengi.
Jaja raia wa Brazil ameonyesha ni mtu mwenye juhudi na
anayependa kujituma na ameshiriki na wenzake bila ya kuonyesha alikuwa na
uchovu wa safari.
Safari
yake kutoka Sao Paulo, Blazil kupitia Johannesburg, Afrika Kusini ilimchukua
zaidi ya saa 12 na nusu lakini leo amekuwa fiti kufanya mazoezini.
Jaja
alishiriki mazoezi ya Yanga leo asubuhi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya
Loyola jijini Dar.
Raha zaidi hakuonyesha ugeni wowote zaidi ya kushiriki vilivyo mazoezi na wenzake.
Mbrazil huyo ameungana na Wabrazil wengine watatu walio katika kikosi cha Yanga ambao ni Marcio Maximo, Leonaldo Leiva na Andrey Coutinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment