ULIMWENGU |
Washambuliaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka
huu) kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao
wamefikia hoteli ya Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu)
watafanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars,
Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao.
SAMATA |
Taifa Stars itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.
Iwapo Taifa Stars itafanikiwa kushinda katika mechi ya kwanza, tena kwa idadi nzuri ya mabao itakuwa imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye mechi ya ugenini mjini Maputo ambayo itakuwa ni ya kurudiana.
0 COMMENTS:
Post a Comment