July 1, 2014



Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amesema yuko tayari kuja kuanza kazi na kikosi chake cha jijini Dar es Salaam.
Loga amesema akiwa kwao Croatia kwamba amejiandaa vya kutosha baada ya kupata mapumziko safi.
“Nimepumzika hapa nyumbani (Croatia), nilisafiri hadi Bosnia, hii ni nchi jirani tu.
“Sasa niko safi kwa ajili ya kazi, nasubiri Simba waniambie lini ninatakiwa ili nije kuanza kazi.
“Niko tayari kabisa na mambo yanakwenda vizuri, nashukuru pia nina afya njema,” alisema Logarusic.
Kocha huyo amekuwa akiamini msimu huu kwa kuwa ataanza kazi kuanzia mwanzo wa msimu basi ana uhakika wa Simba kufanya vizuri kuliko msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic