August 9, 2014

RAMA BAADA YA KUWASILI DAR NA KUPOKEWA NA KIONGOZI WA SIMBA AITWAYE MEDDY.

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema atampa nafasi mshambuliaji Jerome Ramatlhakwane katika mechi ya leo dhidi ya Zesco ya Zambia.

Loga amesema Ramatlhakwane raia wa Botswana ni kati ya wachezaji asiowajua lakini ameamua kumpa dakika 45.
Sijajua kama yuko fiti na amefika hakuweza kufanya mazoezi, hivyo ntampa dakika 45 ili nianze kumuona.
Lakini hiyo haitakuwa mwisho, nitaendelea naye mazoezi ili kujua nini cha kufanya.
Ramatlhakwane ni mshambuliaji wa TP Mazembe anayekipiga kwa mkopo Don Bosco ya DC Congo pia na ndiye mshambuliaji tegemeo zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya Botswana.
Yuko nchini kuangalia nafasi ya kujiunga na Simba inayojiandaa kwa msimu mpya wa 2014-15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic