Mazoezi ya Yanga
yamegeuka kuwa kama ya jeshi, kufuatia kuimarishwa kwa ulinzi ambapo takriban
mabaunsa 15 kutoka matawi mbalimbali ya klabu hiyo wamekuwa wakitanda katika
mazoezi hayo.
Imeelezwa kuwa, Umoja wa Matawi ya
Yanga Dar es Salaam, ndiyo ulioamua kuweka ulinzi mkali kwa kikosi chao ili kudhibiti
mashabiki kuingia uwanjani hapo kinyume na sheria za shule hiyo.
Mmoja wa mabaunsa hao, Maya Mtiga
kutoka Tawi la Manzese, amesema ni makubaliano ya matawi yote Dar ambapo kila
tawi hutoa mwanachama mmoja au wawili kila siku kwenda kulinda hali ya usalama
wa timu yao.
“Sisi tunaruhusiwa kupita pale getini
kwa kuonyesha kadi na hata walinzi wa pale wanajua tunakuja humu kufanya kazi
gani,” alisema Mtiga.
0 COMMENTS:
Post a Comment