Katika kuhakikisha inaondokana na
migogoro ya kiusajili, Mbeya City inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres kupitia betri za magari za RB imeamua kuwasilisha mapema majina ya usajili
wa wachezaji wake wote katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Kuna wachezaji kadhaa wa Mbeya City
wamekuwa wakitakiwa na timu mbalimbali ambapo uongozi wa timu hiyo uliamua
kuwatilia ngumu ikiwa ni pamoja na kuwaongezea dau.
Katibu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, amesema tayari wameshakamilisha usajili
kwa kusajili wachezaji wanne ambao ni Themi Felix, Peter Mwalianzi, Erick
Mawala na Lamboni Asheri na kudai kuwa tayari wameshayawasilisha majina yao TFF.
“Tumeshakamilisha usajili wa wachezaji
wetu wanne tuliowasajili na tayari majina yote ya wachezaji wetu tuliowasajili
tumeshayawasilisha TFF tayari kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu.
“Timu inatarajia kuingia kambini
Agosti 15 tayari kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu, kuhusu mechi
za kirafiki tunamsubiria kocha Juma Mwambusi atoe mapendekezo ya mechi
atakazozihitaji ili tuweze kumtafutia,” alisema Kimbe.
0 COMMENTS:
Post a Comment