August 14, 2014



Kocha Patrick Phiri amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kumuamini kwa mara nyingine.
Lakini amewashauri kutokuwa na haraka kwa kuwa anahitaji kukijenga kikosi.

Phiri ameiambia SALEHJEMBE, anaamini ana nafasi ya kukijenga kikosi chake kutokana na muda alionao.
"Hapa si mgeni, najua watanipa muda na kuniamini ili nikijenege kikosi kwa ajili ya mabadiliko," alisema Phiri.
Kocha huyo mtaratibu, kikosi chake kinasifika kwa soka la pasi za haraka haraka.
Phiri pia ni kati ya makocha waliowahi kuifundisha Simba kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuipa ubingwa bila ya kupoteza hata mechi moja.
Anatarajiwa kusaini mkataba leo kwa ajili ya kuanza kuinoa timu hiyo ambayo siku chache zilizopita, ilimtupia viragp Mcroatia, Zdravko Logarusic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic