August 28, 2014

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI


Wakati TFF ilikuwa ifunge usajili wa Ligi Kuu Bara usiku huu, taarifa inasema siku mbili zimeongezwa.

Kuna taarifa Shirikisho hilo limeamua kuongeza siku mbili za usajili sasa utafungwa tena Ijumaa saa 6 usiku.
“Kuna taarifa kwamba usajili umesogezwa mbele, tumepata taarifa kupitia simu,” alieleza kiongozi mmoja wa klabu usiku huu.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa tayari Yanga na Simba zilishawasilisha majina ya wachezaji wao watano wa kigeni.
Yanga iliwasilisha majina ya Wanyarwanda wawili (Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima), Wabrazil wawili (Jaja&Coutinho) na Hamis Kiiza huku ikiwa imemtema Okwi.
Wakati Simba iliwasilisha majina ya Wakenya wawili (Modo Kiongera&Donald Musoti), Warundi wawili (Amissi Tambwe&Peirre Kwizera) na Mganda, Joseph Owino.
Bado haijajulikana sababu hasa za TFF kuamua kusogeza mbele kwa siku mbili usajili huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic