Pamoja na kufunga mabao
mawili, Gareth Bale ameuponda kinoma Uwanja wa Taifa wa Andorra akisema ni bomu
kuliko yote aliyowahi kuitumia katika maisha yake.
Akiwa na timu yake ya taifa
ya Wales, Bale alifunga mawili na kuiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
ikiwa ugenini.
Mechi hiyo ilikuwa ya
kuwania kucheza michuano ya Euro 2016.
Bale alisema ilikuwa kazi
kumiliki mpira, pia ilimuwia vigumu sana kuweza kupiga mpira uende unapotakiwa.
“Wakati mwingine ulidunda
na kwenda sehemu ambayo si sahihi huku raba nyeusi zikiruka juu, uwanja wa
ajabu kabisa,” alisema Bale ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kusajiliwa na Real Madrid kwa pauni milioni 86 akitokea Tottenham.
0 COMMENTS:
Post a Comment